RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amewasili wilayani hapa mkoani Geita ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.

Rais John Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa wakati alipowasili mjini Chato mkoani Geita kwa ajili ya kukabidhi nyumba za watumishi wa sekta ya afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amewasili wilayani hapa mkoani Geita ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.

Mkapa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe, Mama Anna Mkapa walipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyekuwa sambamba na mkewe, Mama Janeth Magufuli.
Katika msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini, Masaharn Yoshida ambaye leo anakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato (AMCOSS). Rais mstaafu, Mkapa anatarajiwa pia leo kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli utakaofanyika katika Uwanja wa Mazaina ulioko mjini

SOMA ZAIDI