Watu 50 wauawa kwenye mapigano Malakal, Sudan Kusini

Dkt Riek Machar na Rais Salva KiirImage copyrightAFP
Image captionUhasama kati ya Dkt Riek Machar na Rais Salva Kiir uliibuka tena Julai mwaka huu
Zaidi ya watu 50 wanaripotiwa kuuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka nje ya mji wa Malakal nchini Sudan Kusini.
Vikosi vya waasi viliendesha mashambulizi kwenye mji huo wa pili kwa ukubwa siku ya Ijumaa, baada ya kuteka vijiji vilivyo karibu.
Hata hivyo serikali inasema kuwa wanajeshi wake wamewatimua waasi hao hatua iliyosababisha maafa mengi.
Sudan Kusini imekumbwa na misukosuko tangu kujipatia uhuru 2011Image copyrightAFP
Image captionSudan Kusini imekumbwa na misukosuko tangu kujipatia uhuru 2011
Msemaji wa waasi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa wana matumaini ya kuteka mji wa Malakal na kuongeza kuwa hakuna matumaini ya kuwepo makubaliano kati ya kiongozi wao Riek Machar na rais Salva Kiir pamoja na kati ya kabila la Nuer na lile la Dinka.

SOMA ZAIDI