FIFA: Argentina bado wababe, Tanzania washuka


ArgentinaImage copyrightAFP
Image captionArgentina wameendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina.
Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu.
Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne.
Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.
Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107.
Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138.
Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.
Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24.

Mataifa 10 bora duniani

1.Argentina
2.Ujerumani
3.Brazil
4.Ubelgiji
5.Colombia
6.Chile
7.Ufaransa
8.Ureno
9.Uruguay
10.Uhispania

Mataifa 10 bora Afrika

31 Ivory Coast
32 Senegal
35 Algeria
38 Tunisia
45 Ghana
46 Misri
49 DR Congo
58 Mali
59 Cameroon

SOMA ZAIDI