Mwinyi Zahera aonyesha udhaifu katika club ya Yanga


Ukiachana na ile ndoto ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kusema kuwa malengo yake msimu huu ni kuchukua mataji matatu kufeli, juzi ameendelea kufeli tena baada ya Simba kutolewa SportPesa CUP.

Awali Zahera aliibuka na kusema kuwa amejiwekea mikakati ya kuhakikisha anachukua makombe matatu ambayo ni Ligi Kuu, Kombe la FA na SportPesa ambalo ameshalikosa.

Haikutosha, mapema baada ya kuondolewa SportPesa na Kariobangi Sharks kwa mabao 3-2, Zahera aliwatakia Simba kheri ya kutwaa taji hilo ili ije iiwakilishe nchi kwa kucheza na Everton.

Ndoto hiyo ya kuwatakia Simba ushindi nayo inakuwa imepigwa chini baada ya kichapo cha mabao 2-1 kwenye mechi ya nusu fainali.

Fainali hiyo ambayo inaenda kuchezwa leo haitakuwa na timu hata moja kutoka Tanzania ambapo timu pekee za Kenya ambazo ni Kariobang Sharks na Bandari zitakuwa zinacheza.

SOMA ZAIDI