Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 17.07.2017 na Salim Kikeke

Virgil van Dijk
Virgil van Dijk amechezea Uholanzi mechi 12
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda bado akahamia Liverpool kwa pauni milioni 60 msimu huu. Mchezaji huyo amesisitiza anataka tu kwenda Liverpool. (Sun)
Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 45 kumtaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Express)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amepigwa picha kwenye Instagram akiwa amevaa jezi ya Atletico Marid na kuandika "mpe salaam zangu Conte". (Mail)
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku, 24. (Sky)
Chelsea wameonywa na Borussia Dortmund kuwa wana wiki moja tu ya kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang. (The Sun)
Pierre-Emerick Aubameyang
Aubameyang alijiunga na Borussia Dortmund kutoka St Etienne in 2014
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anadhani kuwa ataweza kumshawishi Alexis Sanchez, kutoondoka Emirates. (Mirror)
Vinginevyo Arsene Wenger anafikikia kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele, 20. (Star)
Arsene Wenger amekata tama ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, na badala yake sasa anaelekeza nguvu katika kumsajili Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Telegraph)
Arsenal pia wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, kuziba nafasi ya Alexis Sanchez ikiwa ataondoka. (Don Balon)
Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya Monaco kumuuza kwenda Arsenal. (Sun)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anakaribia kuhamia Juventus kwa pauni milioni 8. (Daily Mirror)
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Star)
Sergio Aguero
Sergio Aguero
Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitano winga wa Atletico Madrid Yannick Carasco, 23. (Don Balon)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka Toni Kroos, 27, kuwa sehemu ya mkataba wowote utakaomhusisha David de Gea kwenda Real Madrid. (Sun)
Manchester United wanaonekana kukaribia kumpata kiungo wa Inter Milan Ivan Perisic. (Daily Mirror)
Zlatan Ibrahimovic amekataa nafasi ya kujiunga na LA Galaxy na anapanga kusaini mkataba mpya na Manchester United. (The Sun)
Ivan Perisic
Ivan Perisic (kulia)
Paris Saint-Germain wanapanga kutoa euro milioni 150 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio. (Don Balon)
AC Milan wananamnyatia mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Gazzetta dello Sport)
Alvaro Morata
Alvaro Morata
Barcelona wapo tayari kutoa euro milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumsajili Marco Verratti kutoka PSG. Calciomercato)
Tottenham wanataka kujaribu tena kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. Timu hizo mbili zimeshindwa kukubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. (Independent)
Tottenham wana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19, mwishoni mwa wiki hii. (Mirror)
Loic Remy, 30, anatazamiwa kuondoka Chelsea msimu huu, huku Everton na Southampton zikimtaka. (Metro)
West Ham watapanda dau la tatu kumtaka winga wa Stoke Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la awali kukataliwa. (Sky Sports)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya
Marko Arnautovic
Marko Arnautovic amechezea Stoke mechi 145
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumatatu njema.

SOMA ZAIDI