hali imekuwatete baada ya nyuki kuvamiaa Mkutano wa chama tawala cha Jubilee nchini kenya

Polisi na msamaria mwema wakijaribu kumsaidia mtu aliyevamiwa na nyuki nje ya mahakama ya juu nchini humoHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPolisi na msamaria mwema wakijaribu kumsaidia mtu aliyevamiwa na nyuki nje ya mahakama ya juu nchini humo
Nyuki walitibua mkutano wa kisiasa wa chama tawala cha Jubilee nchini Kenya katika kaunti ya Taita-Taveta yapata kilomita 360 kutoka mji mkuu wa Nairobi kulingana na gazeti la The Standard.
Wafuasi wa chama hicho walilazimika kukimbilia usalama wao wakati nyuki hao walipowavamia , lakini wakapotea baada ya maombi kufanywa na mwanasiasa mmoja.
Wanasiasa walilaumu shetani kwa uvamizi huo wa mkutano huo uliofanyika katika mji wa Wundanyi ,ulioitishwa kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
Mahakama ya juu nchini humo ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo tarehe 8 mwezi Agosti ikisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na mkosa chungu nzima ikiwemo udanganyifu.
Nyuki wengine waliwavamia maafisa wa polisi na watu wengine nje ya mahakama katika mji mkuu wa Nairobi , wakati majaji walipotoa uamuzi wao kamili kuhusu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo tarehe 20 mwezi Agosti.

SOMA ZAIDI