Watu kadhaa wauawa Jamhuri ya Afrika ya kati CAR


Vikosi vya umoja wa mataifa
Image captionVikosi vya umoja wa mataifa

Maafisa wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wamesema kuwa watu kadhaa wameuawa kufuatia mapigano makali miongoni mwa makundi ya waasi .
Umoja wa Mataifa unasema kuwa makabiliano kati ya makundi hayo yalifanywa katika kijiji kimoja kilichoko kilomita 350 Kaskazini mwa mji mkuu wa Bangi.
Msemaji wa afisi ya aais, Albert Mok-Pene, alisema kuwa watu 26 waliuawa katika kijiji cha Ndomete.
Alisema wanachama wengi wa kundi la Waislamu la Seleka walikuwa wakienda katika kila nyumba wakiwaua wapinzani wao na familia zao.
Alisema kuwa chifu wa kijiji cha Ndomete alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Waasi wa Seleka walimpindua rais wa wakati huo, Francois Bozize mwaka 2013.
Wakristo walijibiza mapinduzi hayo kwa kuwashambulia Waislamu.

SOMA ZAIDI