Sheria za hali ya tahadhari Ethiopia zafichuliwa

Sheria za hali ya tahadhari nchini Ethiopia zafichuliwa
Image captionSheria za hali ya tahadhari nchini Ethiopia zafichuliwa
Serikali ya Ethiopia imefichua sheria mpya zilizowekwa kwa lengo la kuimarisha hali ya tahadhari iliotangazwa wiki iliopita kufuatia maandamano ya ghasia.
Wanadiplomasia hawaruhusiwi kusafiri zaidi ya kilomita 40 kutoka mji mkuu wa Addis Ababa,na amri ya kutotoka nje imewekwa katika viwanda,mashamba na taasisi za serikali.
Ubebaji wa bunduki pamoja na vifaa vinavyoweza kushika moto umepigwa marufuku katika maeneo ya mipakani ambayo yametajwa kuwa maeneo hatari.
Mawasiliano na wanajeshi wa kigeni pia yamesitishwa.
Mamia ya watu wameuawa wakati wa maandaamano ya makabila mawili makubwa nchini Ethiopia ambayo yanadai kuwa yamekandamizwa kisiasa na kiuchumi.

SOMA ZAIDI