Exclusive: List ya wachezaji 5 wazawa wanaomvutia Bokungu




Katika mishemishe za hapa na pale shaffihdauda.co.tz imekutana na beki wa kulia wa Simba Janvier Besala Bonguku na kupiga nae story mkongwe huyu wa soka barani Afrika.
Miongoni mwa vitu ambavyo nilimuuliza ni pamoja na wachezaji watano (5) wazawa anaowakubali wanaocheza ligi kuu Tanzania bara.
“Sijawachunguza sana ila kwa niliowaona hadi sasa, wanaonivutia ni 1. Simon Msuva (Yanga), 2. Ibrahim Ajib (Simba), 3. Aishi Manula (Azam FC), 4. Mohamed Samatta (Tanzania Prisons) na 5. Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar).”
“Wanaweza kuwa wengi lakini hao ni baadhi ya wachezaji ambao wananivutia kwa namna ambavyo wanacheza.”
Bokungu ni mchezaji aliyepata kucheza kwa mafanikio kwenye vilabu vya Esperance ya Tunisia na TP Mazembe ya Congo DR vyenye majina makubwa kwenye soka la Afrika.

SOMA ZAIDI