Marufuku ya laptopu yaondolewa mashirika 2 ya ndege yanayoelekea Marekani
![]() |
| Marufuku ya laptopu yaondolewa mashirika 2 yanayoelekea Marekani |
Mashirika hayo mawili yalisema yameshirikiana na maafisa wa Marekani kuimarisha usalama kwa ndege zinazotoka nchini Kuwait na Jordan.
Marekani ilitangaza marufuku hiyo mwezi Machi kwa safari za moja kwa moja kutoka nchi nane za kiislamu kutokana na hofu kuwa mabomu yangebebwa ndani ya vifaa hivyo.
Mashirika ya ndege ya Etihad, Turkish Airlines, Emirates and Qatar yaliondolewa marufuku hiyo wiki iliyopita.
- Marekani yapiga marufuku laptopu na tabiti kutoka mataifa 8
- Uingereza yapiga marufuku laptopu ndani ya ndege kutoka nchi 6
- Marekani yazuia abiria kubeba laptopu kutoka Misri na Morocco
Shirika la Royal Jordanian ambalo hufanya safari katika miji mitatu ya Marekani kutoka Amman, mji mkuu wa Jordan, liliondoa marufuku hiyo baada ya hatua mpya za kiusalama zilizochukuliwa kwenye ndege zinazoelekea nchini Marekjni.
Shirika linalomikiw na serikali la Kuwait Airlines ambalo hufanya safari zake kutoka Kuwait kuenda mjini New York likipitia Ireland lilisema kuwa marufuku hiyo ilitolewa baada ya maafisa wa Mareknian kukagua usalama kwenye safari zake.

Post a Comment