Muungano wa Saudia: Qatar ni tishio la usalama
![]() |
| Mataifa manne ya kiarabu, yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya Doha ni tishio la usalama |
Mataifa manne ya kiarabu,
yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya
Doha kukatalia mbali masharti hayo magumu dhidi yake, inaashiria nia
yake ya kuendeleza sera ya kuhujumu usalama, katika eneo la mataifa ya
Ghuba.
Kupitia taarifa ya pamoja, Saudia , Milki za kiarabu Misri
na Bahrain, zimeonya kuwa, zitatoa hatua nyingine mpya na ngumu zaidi
dhidi ya Qatar. Mataifa hayo manne yalikatisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar mwezi uliopita, yakidai kuwa, taifa hilo linafadhili makundi ya kigaidi duniani, kama vile kundi la Muslim Brotherhood nchini Misri, na linashirikiana na hasimu mkuu wa Saudi- Iran.
- Qatar yakataa kuafikia masharti iliowekewa
- Misri, Saudi Arabia na Bahrain kufunga anga zake kwa ndege za Qatar
- Mataifa ya Kiarabu yajitenga na Qatar
- Qatar yakataa kuafikia masharti iliowekewa
Qatar imerudia mara kadhaa kuwa, orodha ya masharti hayo, hayana maana kabisa, mojawepo ikiwa kufunga shirika lake la habari la Al Jazeera.

Post a Comment