RONALDO NAYE AMZUIA NEYMAR KUONDOKA BARCELONA
BAADA mastaa Lionel Messi na Luiz Suarez kumweka chini mwenzao, Neymar asiondoke Barcelona, nyota kadhaa wamezidi kujitokeza ili kumsihi asiondoke. Safari hii aliyejitokeza ili kumpa darasa straika huyo ni Cristiano Ronaldo ambaye amemtaka Mbrazil huyo kutokubali kuhama kwa ada hiyo itakayovunja rekodi ya usajili dunia kwa kwenda kujiunga na Paris Saint-Germain. Ronaldo alisema jana kwamba tayari ameshampigia simu staa huyo wa timu mahasimu wao, Barcelona akimueleza kuwa atakuwa amefanya makosa makubwa endapo ataamua kwenda kucheza soka nchini Ufaransa. Mbali na hilo, staa huyo wa Real Madrid alisema pia katika mazungumzo yao hayo alimshauri Mbarazil huyo akajiungea na Manchester United endapo ana dhamira ya dhati ya kuitosa klabu hiyo ya Nou Camp. Inaelezwa kwamba nyota huyo wa Real Madrid, Ronaldo na Neymar wana urafiki wa karibu sana licha ya kuwawanachezea timu pinzani na uhusiano huo ulikua zaidi wakati wawili hao wakiwa chini ya udhamni wa Kampuni ya Nike na jarida moja la michezo nchini Hispania, Diariogol liliripoti kuwa nyota hao wamekuwa wakipigiana simu ili kujadili dau hilo la pauni milioni 192 alilotangaziwa Neymar ili akajiunge na PSG. Jarida hilo lilieleza kuwa katika majadiliano hayo, Ronaldo amekuwa akituma ujumbe mara lkadhaa kupitia mtandao wake wa WhatsApp akimuonya staa huyo mwenye umri wa miaka 25 asiondoke kwenye michuano ya La Liga na kwenda kujiunga Ligue 1 kwa kile anachodai atakuwa amepoteza mwelekeo. Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/ronaldo-naye-amzuia-neymar-kuondoka.html
Copyright © saluti5
Post a Comment