MATIC AANZA KUTAFUTA MAKAZI MAPYA JIJINI MANCHESTER
STAA mpya wa Manchester United, Nemanja Matic juzi aliamua kuitumia siku yake ya kuzaliwa kwa kuzunguka katika jiji la Manchester akiwa na mkewe, Aleksandra ili kutafuta makazi mapya. Staa huyo alimiza umri wa miaka 29 juzi wakati akitafuta pia nyumba mpya katika eneo la Cheshire ambako anataka aishi na familia yake baada ya kuingia mkataba na mashetani hao wekundu.
Kwa mujibu wa gazeti la Dail Mail, mchezaji mwenzake, David de Gea ndiye aliyekuwa wa kwanza kumkaribisha baada ya kutuma ujumbe kupitia katika mtandao wake wa kijamii akimtakia kila la kheri katika siku ya kuzaliwa kwake.
Post a Comment