West Brom wamnunua Gareth Barry kutoka Everton

Gareth BarryWest Brom wamemnunua kiungo wa kati wa zamani wa England Gareth Barry kutoka Everton kwa bei ambayo haijafichuliwa.
Mchezaji huyo wa miaka 36 amecheza mechi 628 katika Ligi ya Premia katika misimu 21 akichezea Aston Villa, Manchester City na Everton.
Anahitaji kucheza mechi tano zaidi pekee kuvunja rekodi ya nyota wa Manchester United Ryan Giggs ya mechi 632.
Barry, ambaye alicheza misimu minne uwanjani Goodison, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja.
Meneja wa West Brom Tony Pulis amesema Barry ni mchezaji mzuri sana na anasubiri kwa hamu sana kufanya kazi naye.
Gareth BarryGiggs alikuwa amecheza katika kila msimu Ligi ya Premia hadi alipostaafu Mei 2014. Alikuwa ameshinda mataji 13 ya ligi akiwa na Manchester United na kucheza mechi 632.
Barry, alicheza mechi yake ya kwanza msimu wa 1997-98 na amecheza zaidi ya mechi 30 kila msimu tangu wakati huo, isipokuwa katika msimu mmoja.
Miongoni mwa wachezaji ambao bado wanacheza, anayemkaribia ni Michael Carrick ambaye amecheza mechi 479.

SOMA ZAIDI