Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu kwa mara ya pili mtawalia.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Aliwashinda Lionel Messi wa Barcelona na mchezaji ghali zaidi duniani anayechezea Paris St-Germain, Mbrazil Neymar.
Messi alimpigia kura mwenzake wa Barcelona Luis Suarez naye Ronaldo alimpigia mwenzake wa Real - Luka Modric.
Meneja wa England Gareth Southgate alimpigia kura Ronaldo.
Wachezaji watatu bora
Cristiano Ronaldo - 43.16 %
Lionel Messi - 19.25 %
Neymar - 6.97%
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLieke Martens
Alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.
Mchezaji bora na meneja bora hupigiwa kura na manahodha wa timu za taifa na mameneja, wanahabari kadha, na kwa mara ya kwanza mwaka huu mashabiki walipiga kura kupitia mtandao.
Kila kitengo cha kura hujumuisha asilimia 25 ya kura zote.
Wachezaji wengine wa kiume waliokuwa wanashindania tuzo hiyo ni:
4: Luka Modric (Croatia, Real Madrid)
5: Toni Kroos (Germany, Real Madrid)
6: Paulo Dybala (Argentina, Juventus)
7: Sergio Ramos (Spain, Real Madrid)
8: Kylian Mbappe (France, Monaco)
9: Robert Lewandowski (Poland, Bayern Munich)
10: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Manchester United)
Post a Comment