DAVID MOYES KOCHA MTARAJIWA WEST HAM BAADA YA SLAVEN BILIC KUTIMULIWA
Kocha Slaven Bilic anatarajiwa kutimuliwa West Ham na nafasi yake inatarajiwa kushikwa kwa muda na kocha wa zamani wa Everton na Manchester United, David Moyes.
Moyes ambaye pia aliikochi bila mafanikio Valencia ya Hispania, ataifundisha West Ham hadi mwishoni mwa msimu.
Uamuzi wa kumtimua Bilic umekuja baada ya West Ham kuwa na mwenendo mbaya msimu huu licha ya kufanya usajili mkubwa.
Kipigo cha 4-1 kutoka kwa Liverpool Jumamosi jioni, kinachukuliwa kama tiketi ya kuhitimisha safari ya Bilic ndani ya West Ham.
Slaven Bilic anatarajiwa kutimuliwa West Ham
David Moyes kuwa kocha mpya West Ham

Post a Comment