Ahukumiwa kunyongwa baada ya kumuua mwenzie




MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mtwara, imemuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa mkazi wa Kijiji cha 
Samora Wilaya ya Newala, Halfani Isumaili Mtepera, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Jafari Selemaini.

Hukumu hiyo imetolewa Ijumaa na Jaji wa Mahakama hiyo, Fauzi Twaibu, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa mashtaka.

Jafari Selemani aliuawa baada ya kushambuliwa na kupewa kipigo kwa madai ya kuiba pampu inayotumika kuwekwa dawa ya kupulizia miche ya mikorosho mashambani, mali ya Shaibu Pepekale.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi, Ally Mkali, aliiomba mahakama hiyo kutowapa adhabu kali wateja wake kwa kile kwa madai ushahidi uliotolewa ulikuwa ukitofautiana.

Jaji Twaibu akitoa hukumu katika kesi hiyo namba12/2015, Ja alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, hivyo akitumia kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhahu sura ya 16 akamuhukumu Selemani adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Hata hivyo,Jaji Twaribu alimuachia huru mshtakiwa wa pili, Juma Mwarabu, kufuatia upande wa mashtaka kushindwa kuithibitishia mahakama hilo shtaka lililokuwa linamkabiri.

Awali ilidaiwa na wanasheria wa Serikali, Mwaija Ahamadi na Emanuel John, kuwa washtakiwa, Khalfani Isumaili Mtopera na Juma Mwarabu, Julai Mosi 2015 katika Kijiji cha Samora Wilaya ya Newala mkoani Mtwara,huku wakifahamu kitendo wanachokifanya ni kosa, walimuua Isumaili kwa madai ya kuiba pampu moja ya kupulizia miche ya mikorosho, mali ya Shaibu Pepekale, mkazi wa kijiji hicho.

Aidha,wanasheria hao walidai baada ya kumuua,washtakiwa hao waliuchoma moto mwili wa marehemu na kutokomea kabla ya kukamatwa.

SOMA ZAIDI