Zari atupa kijembe kwa Diamond, ‘Utakoma tu’

Mambo bado ni mazito kwa ile couple iliyokuwa na nguvu mjini, Diamond na Zari. Baada ya Zari kutangaza kumbwaga muimbaji huyo drama zimekuwa zikiendele bila kusimama.

Zari The Boss Lady ametumia mtandao wa Snapchart kuweka video ambayo unasikika wimbo wa Diamond uitwao Sikomi kisha kuweka caption iliyosomeka ‘Utakoma tu mwenzangu’
Hapo jana Diamond pia aliweka video ya ngoma hiyo katika mtandao wa Instagram na kuandika; ‘Unajua Nyimbo zingine Unaziimba ila Hata we mwenyewe zinakuingia Baadaye’.
Video Player
00:00
00:15
Jumatano ya wiki hii katika siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’.

SOMA ZAIDI