Juma Nature Awaponda Wasanii Chipukizi......."Wakongwe tumesharudi, hatuwezi kukubali "


Msanii mkongwe na miongoni mwa waasisi wa muziki wa BongoFleva, Juma Nature amefunguka na kuwaonya wasanii wa sasa kuacha tabia ya kuigana na kubweteka katika kufanya kazi zao kwa kuwa kitendo hicho kinapelekea kuua muziki.

Juma Nature ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha  EATV baada ya kuwepo minong'ono mingi kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini kulalamikia vitendo vya baadhi ya wasanii kutokuwa wabunifu katika ufanyaji kazi zao

"Hii ni kazi lakini wengine wanachukulia ubishoo. wasanii wanabweteka sana na hilo ndio tatizo kubwa la vijana wa sasa hivi akitoa nyimbo moja anajiona ameshaweza kila kitu. Nawaambia kitu kimoja kwamba wakongwe tumesharudi na hatuwezi kukubali kuona wanakuja watu wengine kutoka sehemu zingine watupite tunawaona hivi hivi, mimi sikubali nasema hata kidogo", amesema Nature.

Pamoja na hayo, Nature ameendelea kwa kusema "sasa hivi wasanii ni wengi sana halafu wengi wao wanaigana ndio maana unakuta hakuna ushindani. Nadhani imefika wakati hawa wasanii wetu kujifunza na kuacha uvivu katika kazi zao za muziki waufanye kazi ambayo itawasaidia wao pamoja na vizazi vyao vitakavyokuja".

Kwa upande mwingine, Juma Nature amesema kilichosababisha wasanii wakongwe 'zamani' ikiwemo yenye mwenyewe ni nyimbo zao kudumu mpaka miaka hii ni kutokana na maudhui ya kazi kutofanana kwasababu kila mmoja wao alikuwa mbunifu.

SOMA ZAIDI