Diamond Platnumz na Rayvanny; wameonyesha kukiri makosa yao mara baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA)

Image result for diamond na rayvanny
Waimbaji kutokea WCB, Diamond Platnumz na Rayvanny wameonyesha kukiri makosa yao mara baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwafungiwa kutojihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana.

Diamond ameeleza kuwa wao kama vijana wamejitahidi kuwa mfano bora siku zote lakini kwa hali ya kawaida kibinadamu lazima makosa yatakuwepo. 

"Japo tunajitahidi kuwa vijana wa mfano bora kwenye Taifa letu, lakini kama tulivyoumbwa binadamu hatuwezi kupatia siku zote, lazma itatokea siku tutateleza tu. Utelezapo, ni vyema kulijua kosa na kulirekebisha ili kesho na Keshokutwa lisijirudie," ameeleza.

"Inshaallah Mwenyezi Mungu Atusimamie na kutuongezea Juhudi na Maarifa katika Kazi zetu ili kwa Pamoja tuzidi kuukuza Muziki wetu na Kuendelea Kuiwakilisha vyema na kulipa sifa Nzuri na Heshima," amemaliza kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Utakumbuka Basata walitoa onyo kali kwa Diamond na Rayvanny kuhusu wimbo wao mpya uitwao Mwanza maarufu kama Nyegezi ambao ulifungiwa na kuamuriwa kutoendelea kuutumia kwenye show zao lakini kwa mujibu wa baraza hilo wasanii hao walikaidi na ndipo adhabu hiyo kubwa ilipowakumba.

SOMA ZAIDI