Mikakati ya Yanga kuhusu ''FA na Ligi Kuu tutapambana tufanye vizuri''



BAADA ya mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara kutolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup hatua ya robo fainali kwa kufungwa mabao 3-2 na KK Sharks, uongozi wa Yanga umesema hasira zao zote zinahamishiwa FA na Ligi Kuu Bara.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wanatambua wamepoteza nafasi ya ushiriki ndani ya SportPesa Cup hali inayowafanya wahamishie hasira zao kwenye mashidano ya FA na Ligi Kuu.

"Tumepoteza SportPesa Cup tunajua kwamba mashabiki wengi wana maumivu hivyo kwa sasa hesabu zetu kubwa ni kwenye michuano ambayo ipo mbele yetu ambayo ni pamoja na FA na Ligi Kuu tutapambana tufanye vizuri.

"Mchezo wetu wa FA utakuwa dhidi ya Biashara United ni timu imara tunaiheshimu ila hamna namna nyingine ya kusema tupo tayari na morali kwa wachezaji ni kubwa ukizingatia tutakuwa nyumbani, ushindi kitu muhimu," alisema Saleh.

SOMA ZAIDI