Wachezaji ''wabaguzi'' kushiriki zoezi na wanawake

Wachezaji wawili wa timu ya soka ya Sparta Prague wameambiwa kufanya mazoezi na timu ya wanawake baada ya kutoa matamshi ya kiubaguzi dhidi ya maafisa wanawake wanaosimamia mechi.
Kipa Tomas Koubek mwenye umri wa miaka 24 alisema kuwa ''wanawake wanafaa kuwa jikoni'' baada ya naibu refa Lucie Ratajova kushindwa kuinua bendera kwa mchezaji ambaye alikuwa ameotea wakati wa mechi ya siku ya Jumapili ambapo ilitoka sare ya 3-3 na Brno.
Kiungo wa kati Lucas Vacha mwenye umri wa miaka 27 alichapisha picha katika mtandao wake wa Twitter ikiwa na matamshi ''waelekee jikoni''.
Afisa mkuu wa klabu ya Sparta Adam Kotalik aliyataja matamshi hayo kama yasio kubalika.
 Tomas Koubek ameichezea mara mbili timu ya Jamhuri ya Czech
Tomas Koubek ameichezea mara mbili timu ya Jamhuri ya Czech

 Refa Mwanamke
                                                                         Refa Mwanamke
 
Akizungumza baada ya mechi ya Jumapili,raia huyo wa Jamhuri ya Czech aliongezea:Wanawake hawafai kusimamia mechi za wanaume.
Baadaye alichapisha picha ya mkewe na mwanawe wa kike katika mtandao wa facebook na kusema ningependa ''kuomba msamaha kwa wanawake wote''.

SOMA ZAIDI