Mosul yakombolewa kutoka kwa wapiganani wa IS

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi akiwapongeza baadhi ya makamanda waliofanikisha ushindi huo
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi akiwapongeza baadhi ya makamanda waliofanikisha ushindi huo
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametembelea mji wa Mosul kuwapongeza wanajeshi katika kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu.
Hata hivyo, hakutangaza rasmi ushindi, akisema hilo litafanyika pindi vikundi vitakapobaki vitakapoondolewa.


Mwanamke huyu na familia yake ni miongoni mwa waliopoteza makazi yao kutokana na vita
Mwanamke huyu na familia yake ni miongoni mwa waliopoteza makazi yao kutokana na vita
Mosul ndipo kundi la wapiganaji wa kiislamu IS lilipotangaza kuunda uongozi wake miaka mitatu iliyopita.Sehemu kubwa ya mji huo imekuwa vifusi baada ya mapigano ya miezi tisa ya kuwaondoa wapiganaji hao.
Muonekano wa mji wa Mosul baada ya vita
Muonekano wa mji wa Mosul baada ya vita
Bwana Abadi amekuwa akitembea katika barabara za mji wa Mosul na kuwapongeza wanajeshi.Wakati huo huo, kumekuwa na sherehe pindi alipozuru eneo hilo.
Mwanzoni kulikuwa na taarifa za kuwepo mapigano, na moshi mzito ukionekana juu ya eneo ambao limekuwa ndio kitovu cha wapiganaji wa IS.
Kundi hilo bado linahodhi sehemu ya magharibi na Kusini mwa Mosul na inaaminika litaendelea kufanya mashambulizi katika sehemu kubwa ya Iraq.
Wanajeshi wa Iraq walipambana usiku kucha kuukomboa mji huo
Wanajeshi wa Iraq walipambana usiku kucha kuukomboa mji huo
Wapiganaji waliuteka mji wa Mosul mwezi June mwaka 2014. Vikosi vya Iraq, vikisaidiwa na mashambulio ya anga kutoka Marekani, vimekuwa vikipambana kuirudisha Mosul tangu tarehem 17 mwezi Oktoba mwaka jana.
Maelfu ya raia wamekimbia huku wengine wakikosa pa kukimbilia wakati mapigano yakiendelea.

SOMA ZAIDI