moto mkubwa uliozuka msituni Canada

Moto huo umesababisha kusambaa kwa moshi mzito ambao ni hatari kwa afya ya binaadamu
Moto huo umesababisha kusambaa kwa moshi mzito ambao ni hatari kwa afya ya binaadamu
Maafisa katika jimbo la British Columbia nchini Canada wamesema wanaweza kuomba msaada kutoka jeshi la nchi hiyo kusaidia kuuzima moto mkubwa uliosababisha zaidi ya watu elfu saba kuyahama makazi yao.
Takriban wazimamoto elfu mbili wanapambana na moto huo uliozuka mwishoni mwa juma huku vikosi zaidi vikiongezwa.
Kwa miaka ya hivi karibuni Canada imekuwa ikikumbwa na majanga makubwa ya moto
Kwa miaka ya hivi karibuni Canada imekuwa ikikumbwa na majanga makubwa ya moto
Ndege za kuzimia moto pia zimetumwa kutoka mji wa jirani wa Saskatchewan.
Siku ya Jumamosi jimbo la British Columbia lilitangaza hali ya hatari kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 14 kutokana na moto huo.

SOMA ZAIDI