Umeshawahi kujiuliza ni Kwanini Hufanikiwi sasa majibu yako haya hapa
Ziko sababu kadha wakadha ambazo nitaziweka bayana kwa lengo la kukufanya ugundue wapi unapokosea hadi hufanikiwi. Upo msemo mmoja unasema “kujua tatizo ni nusu ya kulitatua” msemo huu una maudhui makubwa sana. Kupitia makala hii nitakufanya utambue ni wapi unakwama na itakuwa rahisi sana kuchukua hatua.
Ni wazi ukiwa msituni unaona miti na sio msitu ila unapokuwa nje ya msitu ni rahisi kuona msitu. Ni yangu matumaini nitahakikisha nakutoa nje ya msituni kupitia makala hii na hatimaye uuone msitu na sio miti kama ilivyokuwa awali.
Zifuatazo ni sababu zinazokufanya husifanikiwe;
Ni wazi ukiwa msituni unaona miti na sio msitu ila unapokuwa nje ya msitu ni rahisi kuona msitu. Ni yangu matumaini nitahakikisha nakutoa nje ya msituni kupitia makala hii na hatimaye uuone msitu na sio miti kama ilivyokuwa awali.
Moja, Hauko Tayari Kujitoa Mhanga. Ndiyo hauko tayari kabisa! Umekuwa unachukua tahathari kubwa kila mara na kujionea huruma. Waliofanikiwa ni watu wa kujilipua baada ya kuamua kuchukua hatua. Sasa wewe mara zote unataka uhakika wa kushinda. Sikia maisha hayako hivyo,wanaoyafaidi maisha ni wale wanaojilipua wakiona fursa wanatumbukia huko bila woga. Wanajua nyuma ya kila shida kuna zawadi hasa baada ya kuitatua. Acha kujiami hivyo ukishaamua tafadhali chukua hatua.
Mbili, Hukomai Mpaka Mwisho. Hufanikiwi kwa sababu unaanzisha mambo makubwa na muhimu kwa maisha yako lakini baada ya muda mfupi umeyacha, umekata tamaa. Mara nyingine umekuwa unaanzisha jambo ukiwa moto kweli lakini baada ya muda mfupi umepoa unakaribia kuganda. Waliofanikiwa walikomaa mpaka wakaona matokeo chanya.
Tabia hii mara nyingi husababishwa na kutokuwa mvumilivu, au utarajiaji wa makubwa ya haraka. Sikia mtanzaniamwenzangu hakuna aliyefanikiwa kirahisi. Wote ambao wamefanikiwa wamepigana kweli kweli na hawakurudi nyuma walipokutana na shida au matatizo walipambana zaidi. Jifunze tabia ya kufanya jambo hadi kuhakikisha linatokea. Acha kuanza hili, kesho lile kesho kutwa lile tena. Hiyo ni tabia ya watoto na ndio maana wakaitwa watoto.
Tatu, Kuridhika Mapema.
Hii pia ni tabia ya wasiofanikiwa inayozidi kuwamaliza. Uongo? Nadhani unalojibu, bila shaka kweli. Acha kuridhika mapema, hapo ulipo sio mahala ulipopaswa kuwepo, una uwezo mkubwa sana na unaweza kufanya makubwa zaidi na kuwa mshindi. Hapo si mahala ulipopaswa uwepo ndio maana kuna muda unajiuliza na kujilaumu kwanini maisha yako magumu. Usiwe kama wale ambao wakifanya kazi wakishalipwa pesa hawaonekani kazini mpaka waishiwe pesa.
Nne, Kukosa Kipaumbele.
Hufanikiwi kwa sababu hupangi mambo yako. Na sio tu hupangi mambo yako bali hupangilii shughuli au ndoto zako kwa kufuata kipaumbele. Ukiwa mtu wa namna hiyo wa kutopanga mambo kulingana na vipaumbele kila siku jiandae kushindwa.
Kaa chini leo, orodhesha mipango na malengo yako kisha anza kuipanga kulingana na kipaumbele, ili ujue ni kipi cha kutangulia kutekelezwa kabla ya kingine. Katika kupanga kipaumbele cha malengo yako zingatia sana umuhimu, uharaka, mazingira na vinginevyo.
Tano, Kupenda Njia ya Mkato.
Hii ni sababu nyingine ya kukufanya usisonge mbele kwa sababu unapenda njia za mkato, au unapenda ubwete au njia rahisi. Katika safari ya mafanikio hakuna “shortcut” ni lazima ujitoe na kujituma sana. Lazima uwe “commited enough” fanyakazi kwa bidii, weka akiba, acha kutegemea ndugu, acha kutegemea kutajirika kwa kucheza kamari au“betting” .
Acha kusubiria bahati, kumbuka bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Punguza kulala mno, acha kujionea huruma, acha kushinda vijiweni, soma sana vitabu, kaa na watu waliofanikiwa, wajibika kwa bidii na usijilinganishe na wengine maana hakuna aliye kama wewe.
Asante kwa kuendelea kufuatilia blogu hii ambayo inazidi kukuhabarisha maarifa muhimu sana katika maisha. Enedelea kuwa nasi na bila shaka ni lazima ufanikiwe. Kaa chini na jitadhimini ni kwa jinsi gani na wewe ni miongoni mwa hayo tuliyoyazungumza hapo juu baada ya kujua chukua hatua ya kuyabadili na kuwa mtu mpya kabisa. Usigope utaweza na utafanikiwa hadi kila watu wakushangae.
Wasiliana nasi kwa maoni na maswali kwa kutumia namba na e-maili hapo chini.
Ni mimi mwalimu wako,
Alex MUSHI.
alexmushi@rocketmail.com
bofya hapa ili kusoma zaidi>>>>>> akonewstz.blogspot.com
Post a Comment