MANCHESTER UNITED YASHINDA 1-0 LAKINI YAKIONA CHA MOTO KWA SOUTHAMPTON Soma zaidi hapa


Wakati firimbi ya mwisho inapulizwa kwenye uwanja wa St Mary, Romelu Lukaku akiwa katikati ya dimba, alipiga magoti na kupiga  ngumi ardhini kuashiria furaha iliyopitiliza.

 Kwa mara nyingine tena mshambuliaji huyo aliamua ushindi ambapo kwake na wachezaji wenzake wa Manchester United walijisikia kama wamevuna ushindi mkubwa kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton ulioisha kwa matokeo 1-0.

 Lukaku alifunga bao hilo dakika ya 20 lakini ni Manchester United ndiyo iliyotandaza soka bovu na kuzidiwa katika muda wote wa mchezo. 

Kilikuwa ni kiwango kibovu kuwahi kuonyeshwa na Manchester United sambamba na umiliki wa hovyo wa mpira na ilikuwa wazi kuwa timu hiyo ilikuwa inaomba mpira uishe.

  Southampton: Forster 6, Cedric 5(Ward-Prowse 6), Yoshida 5, Hoedt 5, Bertrand 5, Romeu 7, Lemina 7; Tadic 5, Davis 6(Gabbiadini 5), Redmond 6; Long 7(Austin 6). Manchester United: De Gea 6, Valencia 6, Jones 7, Bailly 6, Young 6, Fellaini 6, Matic 6, Mata 6(Herrera 5), Mkhitaryan 6(Smalling 5), Rashford 6(Blind 5), Lukaku 8.

SOMA ZAIDI