Tetesi za sola Ulaya Jumamosi 04.11.2017


Antonio Conte na mmiliki wa Chelsea AbrahamovicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntonio Conte na mmiliki wa Chelsea Abrahamovic

Hatma ya mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte's huenda haijulikani iwapo kikosi chake kitashindwa na klabu ya Manchester United siku ya jumapili.
Conte amethibitisha kuwa mkufunzi wa Chelsea Abramovich alihudhuria kipindi cha mazoezi huku kukiwa na ripoti kwamba bilionea huyo amechoka kumvumilia Conte. (Metro)
Real Madrid wako tayari kushindana na Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Phillipe Countinho 24. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mabingwa wa Uhispania Real Madrid wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 21. (Marca)
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona Robert Fernandez alikuwa akimsaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 25, wakati Spurs ilicheza dhidi ya Real Madrid katika kombe la vilabu bingwa lakini badala yake alifurahishwa na kiungo wa kati ,21, Harry Winks. (Evening Standard)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola hajachoka kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez 28. (Daily Mail)
Kiungo wa kati wa Chelsea ba Spain Cesc Fabregas, 30, anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya katika uwanja wa Stamford Bridge, na hivyobasi kumaliza uvumi kwamba anaelekea Manchester United. (Evening Standard)
Sunderland wamewasiliana na aliyekuwa mkufunzi wa Middlesbrough Aitor Karanka kuhusu wadhfa wa meneja wa timu hiyo. (Sun)
Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 25, anaendelea kuonyesha kwamba ndio mchezaji bora kuwahi kusajiliwa msimu huu kulingana na beki wa zamani wa klabu hiyo Jamie Carragher. (Telegraph)
Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche amesisitiza kuwa hakuna mtu aliyezubaishwa na uvumi unaoendelea ambao unamuhusisha na Everton. (Burnley Express)

SOMA ZAIDI