yanga leo wa wanusurika kufugwa na singinda united watoa suluhu

Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Singida United na mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga umemalizika katika Uwanja wa Namfua kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.
Katika mchezo huo uligubikwa na utata dakika ya 54 ya kipindi cha pili baada ya mchezaji wa Singida United, Salum Kipaga kupiga mpira kwa kichwa na kuonekana kuingia ndani ya nyavu za Yanga huku muamuzi kuamuru sio bao kufuatia kuonekana kuwa wavuwake umechanika na mpira huo ulipita nje kabla ya kuingia ndani ya goli.
Katika michezo mingine iliyochezwa leo Njombe Mji imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Mbao FC, timu ya Ndanda FC ikiwa nyumbani imetoka suluhu ya bila kufungana na Mtibwa Sugar huku Kagera Sugar ikikubali kulazimishwa sare ya bao 1-1 ikiwa nyumbani dhidi ya Tanzania Prison.
Hapo baadae majira ya saa 1:00 usiku Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC itashuka dimbani Azam Complex kucheza dhidi ya Ruvu Shooting huku.
Baada ya mechi nne za VPL zilizopigwa leo, Yanga imekaa tena kileleni mwa msimamo wa ligi. Hii ni kabla ya mchezo wa Azam FC dhidi ya Ruvu Shooting

SOMA ZAIDI